Okrah rasmi Yanga

WINGA wa zamani wa Simba SC, Augustine Okrah ametambulishwa rasmi kuwa mchezaji wa Yanga.

Nyota huyo mwenye uwezo wa kucheza winga zote mbili, ametambulishwa akiwa Visiwani Zanzibar ambako Yanga inashiriki Kombe la Mapinduzi.

Okrah aliwahi kusajiliwa na Simba SC misimu kadhaa iliyopita hata hivyo hakudumu na timu hiyo.

Huenda Okrah akawa sehemu ya wachezaji wataocheza Kombe la Mapinduzi.

Habari Zifananazo

Back to top button