BAADA ya kukamilisha usajili wa kuitumikia klabu ya Erbil SC ya Iraq, mshambuliaji wa Uganda ‘The Cranes’ Emmanuel Okwi, anakuwa mchezaji wa nne Mganda kuitumikia klabu hiyo.
Wachezaji wengine ambao wamewahi kuitumikia timu hiyo ni Sula Matovu, Ivan Bukenya na Allan Kateregga.
Nyota huyo wa zamani wa Simba SC, ameingia katika orodha ya wachezaji hao baada ya kukamalisha usajili wa kuwatumikia mabingwa hao mara nne wa Ligi Kuu nchini Iraq akitokea Klabu ya Zawraa SC.
Baadhi ya timu nje ya Uganda ambazo Okwi amechezea ni Simba SC, Young African, Etoile Du Sahel (Tunisia), Sonderjyske (Denmark) na Al Ittihad (Misri).