Ole Sendeka: Jumatatu nataja wezi

DODOMA; MBUNGE wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka amesema Jumatatu atawataja wezi waliohusika na upotevu wa pesa za Kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), na Standard Gauge Railway (SGR).

Ole Senderka ameyasema hayo leo Novemba 4, 2023 Bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hoja za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji ya Mitaji ya Umma (PIC).

“Mimi nigekuwa Waziri miezi sita hii hakuna ambaye angebaki aliyetuhumiwa kwenye wizara yangu, lakini nataka niwaambie wako watu wamefisadi kuanzia IPTL leo wako Serikalini”amesema na kuongeza

Advertisement

“Pamoja na maazimio ya bunge, ni leo tu nanyamaza, keshokutwa [Jumatatu] katika mjadala mwingine nitataja nani wako nyuma ya IPTL, nani yupo nyuma ya ufisadi wa SGR ambayo manunuzi  yametugharimu hasara,”amesema Ole Sendeka.

Amesema kwa ufisadi uliofanyika, pesa zingetolewa, kwenye miradi ya maendeleo Zanzibar ingepata gawio la zaidi ya Sh bilioni 300.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *