Omondi amkalia kooni Diamond chanzo Tanasha
DAR ES SALAAM: NYOTA wa uchekeshaji, Erick Omondi amesema Kenya hawataki pesa kwa Diamond Platnumz badala yake wanataka ng’ombe 500 kama mahari ili amuoe mzazi mwenziye, Tanasha Dona.
Omondi, ameeleza hayo leo alipotua katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere kuhudhuria uzinduzi wa kipindi cha Runinga cha maisha halisi ‘Reality Show’ cha msanii wa bongo fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ kitakachozinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
“Kama familia ya Tanasha, mimi kaka yake tumemwambia Diamond Platnumz kuwa hatutaki pesa,” amesisitiza nyota huyo kutoka Kenya.