Onana arejesha furaha Simba

TANGA: Simba wameondoka na alama zote tatu kwa kuitandika Coastal Union 2-1 mchezo uliomazika muda mchache uliopita Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga.

Ushindi huo umemfanya Mnyama Simba kufikisha alama 39 baada ya michezo 17 akiwa katika nafasi ya tatu kwenye msimamo.

Mabao ya Simba katika mchezo huo yamewekwa kimyani na Freddy Michael ’11’ na Willy Onana ’83’ huku goli la kufutia machozi kwa Wagosi wa Kaya Coastal Union likifungwa na Lucas Kikoti ’24’

 

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button