Onana tayari huko

IMERIPOTIWA kutoka kwa mwandishi wa habari za michezo nchini Italia, Fabrizio Romano kuwa kipa Andre Onana atasafiri leo kwenda jiji la Manchester kufanya vipimo vya afya na kuandaa karatasi za mkataba tayari kujiunga na United.

Romano amesema Mcameroon huyo atawasili katika jiji hilo saa moja kwa saa za England na huenda usajili wake kutoka Inter Milan kwenda United ukakamilika leo au kesho.

Mbobezi huyo wa masuala ya usajili ameeleza dau la €51m na nyongeza ya €4m ndilo linalomng’oa Onana Inter Milan.

Mkataba wa miaka mitano wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja umeandaliwa kwa ajili ya nyota huyo kusaini.

Habari Zifananazo

Back to top button