KIPA Andre Onana anakaribia kujiunga na Manchester United, baada ya jana usiku Inter Milan na United kufikia makubaliano ya mwisho.
Imeelezwa kutoka kwa Fabrizio Romano kuwa baada ya makubaliano hayo kinachofuata ni kuandaa karatasi za mkataba baada ya hapo wataomba kumfanyia vipimo vya afya.
Romano amesema Onana atasaini mkataba wa miaka mitano utakaomuweka Old Trafford hadi Juni 2028 wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja.
Amesema United itamtangaza kipa huyo wiki hii.