Opa atambulishwa Besiktas
ALIYEKUWA mshambuliaji wa Simba Queens, Opa Clement leo ametambulishwa rasmi katika klabu yake mpya ya Besiktas ya wanawake ya nchini Uturuki.
Kupitia ukurasa rasmi wa hiyo imeeleza kuwa nyota huyo amefaulu vipimo vya afya katika Hospitali ya Fulya na hivyo kuingia rasmi mkataba na timu hiyo.
“Usajili wetu mpya Opa Clement amejiunga na mazoezi kwa mara ya kwanza na timu yetu”. Imeeleza taarifa hiyo