Osimhen atwaa tuzo mchezaji bora Afrika

STRAIKA wa Napoli na timu ya taifa ya Nigeria, Victor Osimhen ameshinda tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wanaocheza nje ya Afrika.

Katika tuzo hizo zinazotolewa leo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Osimhen amewashinda Hachraf Hakimi wa Morocco na Mohamed Salah kutoka Misri.

Tuzo hiyo imetokana na ubora wa msimu uliopita wa mchezaji huyo ambapo akiwa Napoli alifunga mabao 29 katika michezo 38 ya Ligi Kuu Italia ‘Serie A’

Sambamba na kufunga mabao hayo, mkali huyo wa kucheka na nyavu aliifanikishia Napoli kushinda ubingwa wa ligi hiyo msimu uliopita.

Aidha kwa upande wa wanawake tuzo ya mchezaji bora imeenda kwa Asisat Osoala wa Nigeria akiwapiku Thembi Kgatlana wa Afrika Kusini na barbara Banda wa Zambia.

Habari Zifananazo

12 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button