Osimhen kuwavaa Afrika Kusini

MSHAMBULIAJI wa Nigeria, Victor Osimhen atakuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza nusu fainali ya Afcon dhidi ya South Afrika leo.

“Victor Osimhen amethibitisha kuwa imara kwa ajili ya mchezo huo, alijiunga na timu Bouake na amefanya mazoezi na timu”.msemaji wa timu hiyo aliambia mtandao wa AFP.

Awali ilikuwa hatihati kwa mchezaji huyo kuwepo katika mchezo huo, na hakusafariki kwenda Bouake Jumatatu baada ya kutojisikia vizuri.

Mchezaji bora huyo wa Afrika alikosa mazoezi Jumatatu, huku akishindwa kumaliza katika mchezo war obo fainali dhidi ya Angola.

Kocha Jose Peseiro alikuwa akikwepa swali juu ya uwezekano wa Osimhen kuikabili Afrika Kusini alipoulizwa katika mkutano na waandishi wa habari mapema jana.

“Siwezi kujibu kwa sasa kwa sababu ni tatizo la kiafya. Leo mchana nitajua vyema kama anaweza kucheza au la”. Alisema

Habari Zifananazo

Back to top button