OUT wajipanga kukabili unyanyasaji kijinsia

MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Profesa Elifas Bisanda amewataka wanafunzi kutoa taarifa zote zinazohusu unyanyasaji wa kijinsia katika vituo walivyopo, ili zishughulikiwe kwa mujibu wa sheria

Profesa Bisanda ametoa wito huo wakati wa kikao cha 42 cha Bunge la Wanafunzi kilichofanyika katika Kituo cha OUT kilichopo mkoani Manyara.

Amesema kwa kutambua umuhimu wa masuala ya kijinsia, OUT imeunda dawati la jinsia kwenye kila kituo cha mkoa, hivyo wameandaa mafunzo jijini Mwanza ya wale watakaokuwa wanahudumia madawati hayo.

” Tunaomba jamani mtusaidie wanafunzi katika kuripoti matukio yote katika mazingira yetu yanayohusu unyanyasaji wa kijinsia baina ya wanafunzi na wanafunzi ama wanafunzi na walimu,” amesema.

Kwa upande wake Waziri wa Jinsia wa Serikali ya Wanafunzi chuoni hapo (OUTSO), Caroline Shoo amesema wamekuwa wakikumbana na matukio ya unyanyasaji wa vijana wa kiume dhidi ya wanawake, hivyo kuwaita na kuzungumza nao.

” Tunakutana na changamoto za vijana wa kiume kuwasumbua wa kike. Hivyo likifika kwetu tunawaita na kuzungumza nao kwa usiri,” amesema.

Amesema pia wamekuwa wakitoa elimu kwa wanafunzi kuwaelimisha ni mambo gani yanaweza kuonekana kuwa ni ukatili.

Habari Zifananazo

Back to top button