Pacome aitanguliza Yanga
KIUNGO Pacome Zouzoua ameipelekea Yanga mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0. Bao hilo limefufua matumaini ya Yanga kufuzu robo fainali.
Pacome amefunga bao hilo dakika ya 33.
Endapo matokeo hayo yatabaki hivyo, Yanga itakuwa na pointi 5 katika nafasi ya pili.
Kinara wa kundi D, Al-Ahly pia ana pointi 5 atacheza usiku huu dhidi ya CR Belouizdad.