Panga pangua baraza la mawaziri Mabula, Masanja watemwa
wapya wachomoza, Kihenzile, Jerry Silaa wachomoza
DAR ES SALAAM: RAIS Samia Suluhu Hassan amepangua Baraza la Mawaziri, huku akimuacha Mbunge wa Ilemela Angelina Mabula ambaye alikuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa.
Pia, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza, Mary Masanja aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii ametumbuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Dunstan Kitandula, Mbunge wa Mkinga.
Aidha, Rais Samia ameteuwa Mawaziri wapya watano na Makatibu Wakuu watatu na Manaibu Watatu.
Akitangaza mabadiliko hayo leo Agosti 30,2023 Katibu Mkuu Kiongozi, Moses Kusiluka amewataja wapya katika baraza hilo la Mawazi ni Jerry Silaa, Waziri wa Nyumba, Maendeleo ya Makazi, David Kihenzile Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Uchukuzi; .Judit’h Kapinga, Mbunge wa Viti Maalum (Ruvuma) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nishati; Alexander Mnyeti, Mbunge wa Jimbo la Misungwi ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.