Panzi mwenye rangi ya Taifa ajengewa mnara Dar

PANZI mwenye rangi sawa na bendera ya Tanzania, anayepatikana katika hifadhi ya mazingira asilia Pugu Kazimzumbwi, Wilaya ya Kisarawe, Pwani amejengewa mnara katika mzunguko uliopo eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam, ili kutoa uelewa kwa Watanzania wamjue.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka, alisema hayo alipokuwa akizungumza na HabariLeo kuhusu vivutio vilivyopo kwenye hifadhi hiyo.

Prof. Sedoyeka alisema katika kutangaza vivutio vilivyopo kwenye hifadhi nchini, wamemchukulia kwa uzito ndio maana wamemjengea mnara huo.

Alisema katika kuhakikisha anaendelea kuwepo panzi huyo, wanamlinda katika mazingira aliyopo.

Mhifadhi Msaidizi kutoka Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Regina Mwakifuna, alisema panzi huyo amekuwa kivutio kikubwa kwa wageni wanaofika katika hifadhi hiyo.

Alisema panzi huyo alianza kuonekana Novemba 20 mwaka 2020.

Alisema amekuwa akionekana zaidi miezi ya Novemba mpaka Aprili, rangi zake ni bluu, nyueusi, njano na kijani, ambazo ni rangi za bendera ya Tanzania.

 

Habari Zifananazo

Back to top button