Pape Sakho aitwa kikosi cha Senegal

Pape Sakho aitwa kikosi cha Senegal

KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Pape Sakho ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Senegal kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali ya Afcon 2023, dhidi ya Msumbiji.

Hiyo ni mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kuitwa kwenye timu ya taifa tangu alipojiunga na miamba hiyo ya Tanzania mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Teungueth ya nyumbani kwao Senegal.

Kwa mujibu wa vyombo vya Habari vya Senegal, vinaeleza kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Aliou Cisse amemjumuisha Sakho baada ya kuvutiwa na kiwango chake akiwa na Simba kwenye michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Advertisement

“Nimchezaji mwenye kipaji cha juu ukitaka kuthibitisha hilo msimu uliopita aliibuka mshindi wa bao bora kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho naamini anaweza kutusaidia kufikia malengo yetu dhidi ya Msumbuji,” alisema Cisse.

Katika orodha ya wachezaji 24, Sakho ataungana na mshambuliaji wa FC Beyern Munich, Sadio Mane, Gana Gueye anayekipiga Everton, Bamba Dieng anayecheza Ligi Kuu ya Ufaransa kwenye klabu ya Lorient FC.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *