Partey kuikosa Liverpool

BAADA ya siku tatu zilizopita Arsenal kutangaza kurejea kwa kiungo Thomas Partey, kocha wa timu hiyo, Mikel Arteta amesema Mghana huyo atachelewa kurudi uwanjani kwani bado hajapona vizuri .

Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa Jumapili dhidi ya Liverpool uwanja wa Emirates, Arteta amesema mchezaji huyo hajajua muda wa mchezaji huyo hasa wa kukaa nje kuuguza jeraha lake.

“Kama ni siku moja au majuma, tutaona. Alihisi kitu tena katika eneo linalofanana”. Amesema Arteta akitoa taarifa za wachezaji wake kuelekea mchezo huo.

Arsenal itaendelea kumtumia Declan Rice kwenye eneo la kiungo ambaye amekuwa akianza katika eneo hilo tangu kuanza kwa msimu huu.

Habari Zifananazo

Back to top button