Partey kusepa Arsenal ?

ARSENAL wapo tayari kumuuza kiungo Thomas Partey, 30, msimu huu. Mtandao wa Telegraph nchini Uingerea umeripoti.

Taarifa ya awali iliyotolewa na mwandishi wa habari za michezo, Fabrizio Romano ilieleza kuwa kuna klabu kadhaa zilizoonesha nia ya kumsajili Mghana huyo.

Taarifa yake ilifafanua kuwa mazungumzo baina ya Arsenal na klabu hizo ambazo hakuzitaja yanaendelea na kuna nafasi ya kiungo huyo kuondoka.

Advertisement

Mkataba wa Partey unamalizika 2025 hata hivyo hakuna mazungumzo yoyote ya Arsenal na Partey kuhusu mkataba mpya.