Pasipoti 10 zenye nguvu zaidi baraani Afrika

WAKALA wa Henley & Partners umetoa ripoti yake ya kila mwaka ya hati za kusafiria zenye nguvu zaidi duniani ambapo nafasi ya kwanza bado inashikiliwa Japan ikifuatiwa na Singapore na Korea Kusini zilizoko bara la Asia.

Kwa Afrika Ushelisheli inaongoza ikiwa ni ya 29 kwa Dunia ikiwa imejikusanyia alama 153. Mauritius imeibuka kuwa nchi ya pili na ya 34 kwa Dunia ikiwa na alama 146.

Nchi ya Tatu ni Afrika Kusini ambayo kwa takwimu za kidunia ni nchi ya 53. Imefuatiwa na jirani yake, Botswana, ambayo iko katika nafasi ya 63.

Namibia imeshika nafasi ya Tano na ya 67, ikifuatiwa na Lesotho iliyo nafasi ya 69, na eSwatini ikisimama nafasi ya 71.  Nafasi ya Nane imechukuliwa na nchi iliyo Mashiriki mwa Afrika, Malawi ambayo kwa tathimini iko nafasi ya 72 kiDunia. Kenya imeibuka nafasi ya 73 ikifuatiwa na Tanzania ambayo imeshika nafasi ya 10 ikiwa namba 74 kwa kuwa na hati ya kusafiria yenye nguvu zaidi.

Pasipoti ya Zambia ni ya kumi na moja kwa nguvu barani Afrika, katika nafasi ya 75, ikifuatiwa na Tunisia (76), Gambia (77), Uganda (78) na Zimbabwe (79). Ghana na Morocco zinashiriki nafasi ya 80, mbele ya Sierra Leone katika nafasi ya 81, Msumbiji (82), Benin na Rwanda (83), Sao Tome and Principe (84) na Mauritania (85).

Pasipoti za Afrika Magharibi zina thamani chini ya hiyo, huku Burkina Faso ikishika nafasi ya 86, mbele ya Côte d’Ivoire, Gabon na Senegal (87). Equatorial Guinea, Guinea, Madagascar na Togo ziko katika nafasi ya 88.

Baadhi ya nchi 21 za Kiafrika zinaanguka kati ya nafasi ya 89 na 101 (pamoja na idadi sawa ya pointi).

Pasipoti ya Kiafrika yenye ushawishi mdogo ni ile ya Somalia, ambayo inashika nafasi ya 104 ikiwa na pointi 35. Pointi saba zaidi ya pasipoti yenye nguvu kidogo zaidi ulimwenguni. Paspoti ya Afghanistan iko katika nafasi ya 109.

Nafasi hiyo inatokana na taarifa zilizotolewa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (IATA), ambalo huhifadhi takwimu za taarifa za usafiri.

Habari Zifananazo

Back to top button