Pato la taifa laongezeka kwa Asilimia 5.2

PATO la Taifa (GDP) mwaka 2023 limeongezeka hadi kufikia asilimia 5.2 mwaka 2023 huku mfumuko wa bei ukisalia katika tarakimu moja.

Akisoma Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2023/2024 na Hali ya Uchumi wa Taifa wa mwaka 202215, 2023 Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba amesema mpango huo umeandaliwa kwa kuzingatia sera na mikakati mali mbali ya kikanda na kitaifa.

“Ukuaji wa Pato halisi la Taifa umekuwa kufikia asilimia 5.2 mwaka 2023 ikilinganishwa na asilimia 4.7 mwaka 2022.” Amesema Mwigulu

Advertisement

Aidha, Mwigulu amesema kuwa licha ya pato la taifa kuongezeka lakini deni la taifa limefikia  Sh trilioni 77  hadi Machi, 2023 sawa na ongezeko la asilimia 11.2 ikilinganishwa na mwaka 2022.

“Hadi Machi 2023, deni la Taifa lilifikia Shilingi trilioni 77  kutoka Sh trilioni 69.3 katika kipindi kama hicho mwaka 2022, sawa na ongezeko la asilimia 11.2.”Amesema

Amesema kati ya kiasi hicho, deni la ndani lilikuwa Shilingi trilioni 26.9  na deni la nje Shilingi trilioni 50.2

Mwigulu amesema, ongezeko la deni hilo lilitokana na kuongezeka kwa mahitaji ya fedha kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege, umeme na maji.