Paulina Onna, Janjaro kumbe walikutana angani

DAR ES SALAAM: MKE wa msanii wa Hip Hop Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ anayeitwa Paulina Onna maarufu ‘Quenlinnatotoo’ameiambia HabariLEO kuwa kwa mara ya kwanza alikutana na mumewe kwenye ndege wakiwa siti moja kuelekea Afrika Kusini.

Quenlinnatotoo na Dogo Janja wamepata mtoto wa kiume Ahyan Abdulaziz mwenye umri wa miezi sita, mwandishi wetu alitaka kujua ilikuaje wawili hao wakakutana pamoja na kuanza safari yao ya maisha.

Akijibu swali hilo Quenlinnatotoo alisema: Mara ya kwanza nilikutana na Dogo Janja uwanja wa ndege tukapanda ndege moja ya kwenda Afrika Kusini na ilivyo bahati tulipangiwa kukaa sehemu moja hivyo tukawa tunapiga stori safari nzima.”

Maongezi yao yalikuwa ya aina gani ndani ya safari hiyo? Quenlinnatotoo hakuweka wazi lakini baadaye walikubaliana kuanzisha uhusiano wa kimapenzi kufunga ndoa.

Amesema baada ya kupata mtoto huyo amepanga kuendelea kupata watoto wengine na mume wake kwani anapenda zaidi watoto: “Kabla ya kuwa na mtoto tayari nina watoto ambao nawatambua kama watoto wangu kwa hiyo hapo kwenye idadi ya watoto sina hesabu nazoweza kukupa napenda watoto nalea watoto wengi zaidi.”

Habari Zifananazo

Back to top button