Pauni ya Uingereza yaanza kuimarika 

Pauni ya Uingereza yaanza kuimarika

PAUNI ya Uingereza imeanza kuimarika baada ya serikali kusema kuwa ilikuwa ikifanya marekebisho ya mpango tata wa kupunguza kodi katika bajeti yake ndogo.

Waziri wa Fedha Kwasi Kwarteng alisema serikali haitaondoa kiwango cha juu cha ushuru wa mapato nchini, kama ilivyoainishwa wiki moja iliyopita.

Pendekezo hilo pamoja na ongezeko lililopangwa la ushuru wa kampuni na mpango ghali wa kutoa ruzuku kwa bili za nishati kwa kaya na biashara ulizusha hali mbaya ya imani kwa serikali, na kupeleka pauni kuanguka na kuathiri dhamana za serikali.

Advertisement