Pele afariki Dunia akiwa na miaka 82

Pele, nguli wa soka wa Brazil na mshindi mara tatu wa Kombe la Dunia, amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 82.

Pele ambaye anachukuliwa kuwa nyota wa kwanza duniani, alikuwa akitibiwa saratani ya utumbo mpana, kufuatia upasuaji wa kuondoa uvimbe uliofanyika Septemba 2021, na alihitaji matibabu ya mara kwa mara.

Baada ya kurudishwa hospitalini mwishoni mwa Novemba ili kutathmini upya matibabu yake ya saratani, aligunduliwa na maambukizi ya upumuaji kabla ya kuhamishiwa kwenye huduma ya matibabu wakati mwili wake uliposhindwa kuitikia matibabu ya mionzi.

Madaktari na wauguzi katika Hospitali ya Albert Einstein huko Sao Paulo wamesema Pale ameaga dunia akiwa hospitali pembeni ya mke wake, Marcia Aoki, aliyekuwa kando ya kitanda cha hospitali.

Aliaga dunia siku ya Alhamisi. Binti yake, Kely Nascimento, alithibitisha habari hiyo kwenye Instagram, akiandika: “Kila kitu tulichonacho ni shukrani kwako.

Tunakupenda sana. Pumzika kwa amani.”

Habari Zifananazo

Back to top button