Pele awahishwa hospitali uvimbe wamtesa
Gwiji wa soka wa Brazil, Edson Arantes ‘Pelé’ ambaye anayedhaniwa kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi wakati wote, amelazwa katika hospitali ya Sao Paulo baada ya kupata uvimbe, matatizo ya moyo na kiakili, vyombo vya habari nchini humo, vinaripoti.
Mtandao wa ESPN Brazil unaeleza kuwa Pele anasumbuliwa na matatizo mengi hali iliyosababisha ashindwe kula wakati akingojea vipimo vya ziada. Pele, ambaye ana umri wa miaka 82, amekuwa akiugua saratani na madaktari wana wasiwasi kuwa tiba yake huenda isiwe tija, taarifa ya ESPN.
Kely Nascimento, binti wa gwiji huyo alipuuza ripoti za vyombo vya habari, amesema ” “Baba yangu amelazwa hospitalini, anadhibiti dawa zake,” alisema kwenye chapisho kupitia Instagram, ambalo halikutoa maelezo maalum.
Pele alilazwa hospitalini Septemba 2021, alipofanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye utumbo mpana na kukaa kwa siku kadhaa katika uangalizi maalum.
Baadaye aliachiliwa huku akiendelea na matibabu.