‘Pelekeni mifugo majosho ya serikali’

Waliogawana mifugo ya watuhumiwa matatani

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Khamis Hamza Chilo, amewataka wafugaji wote nchini kupeleka mifugo yao katika majosho ya serikali yaliyojengwa katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuzisaidia jamii zilizoathirika na mabadiliko ya tabia nchi.

Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na jamii ya wafugaji katika Kijiji cha Machenje, wilayani Kongwa jijini Dodoma leo Januari 19, 2023.

“Tunaomba wananchi wote wanaomiliki mifugo yote ya miguu minne, wa maeneo haya na maeneo mengine yote Tanzania waende wakawakoshe wanyama wao kwenye majosho haya ya serikali vinginevyo tunadhulumu wanyama hawa kuwa salama dhidi ya maradhi,”

Advertisement

Aliwaonya wananchi juu ya ukataji miti hovyo na kuwaasa kupanda miti ili wanyama waweze kupata chakula na maeneo ya kupumzika.

“Maeneo ni ya jangwa na ni kwa sababu watu wamekata miti sana, wanyama hawa wakitoka kwenye majosho wanahitaji chakula na vyakula vya wanyama sio nyama hasa hawa ng’ombe, vyakula vyao ni majani. Ipandeni miti ili wanyama wetu hawa pamoja na sisi wapate vivuli, lakini pia wapate majani ya kula,” alisema naibu waziri.

Pia aliwashauri wafugaji kuacha tabia ya kupiga wanyama mpaka kuelekea kuwatoa vidonda na kuwasihi kuwachunga kwa busara na katika hali ya kujali, huku akisema na wao ni viumbe hai.

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *