Pence akana kutaka kuwania urais

Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani, Mike Pence hajawasilisha ombi la kugombea urais mwaka 2024 kwa mujibu wa mshauri wake, Devin O’Malley alisema kwenye Twitter, baada ya taarifa inayodaiwa kuwa Pence alionekana kwenye tovuti ya Tume ya Uchaguzi akijaza fomu ya kuutaka urais.

Vyombo vya habari likiwemo Shirika la Habari la Sky News la Uingereza liliripoti kwamba Pence aliwasilisha fomu ya kugombea urais, kwenye tume ya uchaguzi.

O’Malley, ambaye alikuwa katibu wa waandishi wa habari wa Pence alipokuwa makamu wa rais, alitweet “Makamu wa Rais wa Zamani Mike Pence hakuwasilisha kugombea Urais leo” na baadaye alithibitisha kwa Reuters kwamba yeye ni mshauri wa Pence.

Advertisement

Msemaji wa Tume ya Uchaguzi (FEC) alisema hawatoi maoni yao kuhusu majalada mahususi, ila alibainisha kuwa Tume inakagua fomu za usajili zinazoweza kuwa za uwongo ili waziripoti.

Pence aliwahi kuwa Gavana wa Jimbo la Indiana na alikuwa Makamu wa Rais (2017-2021) chini ya uongozi wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Donald Trump.