Pensheni wastaafu Zanzibar sasa asilimia mia

RAIS  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Mwinyi amepandisha pensheni ya wastaafu Zanzibar leo Mei Mosi, 2023 ambapo kima cha chini imeongezeka kwa asilimia 100 na wastaafu wengine ikiongezeka kwa asilimia 150

Rais Mwinyi,  ametangaza kupandishwa kwa kima hicho cha pensheni katika maadhimisho ya Mei Mosi yanayoendelea kwenye viwanja vya Nungwi visiwani humo.

Pia, amesema pia, serikali ipo kwenye hatua za mwisho za kuanzisha mfumo wa Bima ya afya kwa wafanyakazi wote wa umma Zanzibar.

Aidha, Rais  Mwinyi amesema serikali imelipokea na inakwenda kulifanyia kazi ombi la wafanyakazi juu ya kupata fedha za nauli zitakazowawezesha kwenda kazini na kurejea majumbani nje na mshahara.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button