MSHAMBULIAJI wa Al-Ahly Percy Tau ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kutoka kwenye mashindano ya vilabu barani Afrika.
Percy Tau ameshinda tuzo hizo za CAF akiwapiku Peter Shalulile wa Mamelodi na Fiston Mayele (Yanga na Pyramids).
Tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kutoka kwenye mashindano ya vilabu kwa wanawake imeenda kwa Fatima Tagnaout wa Morocco akiwapiku Refilwe Tholakeke wa Botswana na Lebohang Ramalepe Afrika Kusini.
Tuzo ya mchezaji bora kijana upande wa wanaume imechukuliwa na Lamine Camara wa Senegal akiwapiku Amara Diouf Senegal na Abdessamad Ezzalzouli wa Morocco.
Tuzo ya mchezaji bora kijana kwa wanawake imekwenda kwa Nesryne El Chad wa Morocco akiwapiku Comfort Yeboah Ghana na Deborah Abidoun wa taifa la Nigeria.
Comments are closed.