Phiri aisogeza Simba mbele

BAO pekee lililofungwa na Moses Phiri limetosha kuivusha Simba SC kutoka nafasi ya tatu hadi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu, baada ya kuifunga Namungo FC bao 1-0 katika mchezo uliopigwa leo Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Phiri amefunga bao hilo dakika ya 32 ya kipindi cha kwanza.

Simba imesogea nafasi ya pili ikiwa na pointi 24, na michezo 11, huku Azam FC ikiwa nafasi ya kwanza ikiongoza kwa pointi 26 na michezo 12. Yanga inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 23 ambapo kesho watacheza na Singida Big Stars Uwanja wa Mkapa.

Michezo mingine iliyopigwa leo, Geita Gold imeshinda mabao 4-2 dhidi ya Tanzania Prison na kufikisha pointi 17 ikiwa nafasi ya sita.

Mtibwa Sugar baada ya kupoteza dhidi ya Azam FC, leo waitandika Coastal Union mabao 2-1 na kufikisha pointi 18 ikiwa nafasi ya tano

Habari Zifananazo

Back to top button