Phiri alindwe kwa namna gani?

Phiri alindwe kwa namna gani?

NIMEZUNGUKA kwenye page tofauti za wadau mbalimbali wa mpira wa miguu, wakiwemo wachambuzi mahiri nchini nimekutana na mjadala kuhusu mshambuliaji wa Simba Moses Phiri alindwe, anachezewa sana rafu. Sawa ni mtazamo yao.

Tuulizane maswali kwanza! Waamuzi wamlinde Phiri kivipi? Ukiondoa mechi ya jana dhidi ya Kagera Sugar kuna mechi nyingine Phiri alichezewa madhambi kulinganisha na jana?

Advertisement

Miaka ile AC Milan vs Manchester United, Cristiano Ronaldo alichezewa rafu nyingi mno hatukuwahi kusikia habari za alindwe,  mechi ya Uholanzi juzi tu hapa Messi wa Argentina alichezewa rafu sana na hatukusikia mambo ya kulindwa.

Tuachane na mifano! Iko hivi kitakachomlinda Phiri ni sheria za soka tu, Sheria namba 12. Foul & Misconduct, kwenye dangerous play opponent atapewa red card na kwenye madhambi ya kawaida basi ataonywa kwa kadi ya njano.

Kwenye suala la Phiri kama alifanyiwa madhambi mwamuzi wa mchezo alitakiwa kuwaadhibu wanaofanya hivyo kwa kadi nyekundu au kadi ya njano tu.Ila kama mwamuzi hakufanya hivyo basi kesi inabaki kwake.-

Ila suala la Phiri kulindwa na mwamuzi halina afya sheria ndo zitamlinda.-

Watu kukabana na kukamiana kwenye mechi sio kitu kigeni, Messi alikuwa mpaka anatamani kulia akikutana na Ramos na Pepe karibu kwenye El-Classico zote walizokutana, lakini mwamuzi akiona imezidi penye kustahili anatoa adhabu, Ramos aliwahi kula umeme dhidi ya Messi na hiyo ndiyo ilikuwa njia ya kumlinda Messi.-

Sasa sijajua Phiri alindwe kwa namna gani? Wachezaji wanalindwa na sheria na kanuni zake tu.