Phiri hana wasiwasi na Baleke

MSHAMBULIAJI wa Simba SC, Moses Phiri hana wasiwasi na usajili mpya uliofanywa na timu hiyo hasa kugombea nafasi ya kucheza na kwamba kwa upande wake yuko tayari kushindana nao labda kwa upande wao.

Phiri ametoa kauli hiyo leo alipowasili Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere akitokea Dubai ambako Simba iliweka kambi ya siku kadhaa.

Kinara huyo wa mabao kwa Simba ameeleza kuwa wachezaji hao wataongeza thamani kubwa kwenye kikosi hicho, na kwamba kwenye timu yoyote lazima kuwe na wachezaji wengi ili kutoa nafasi ya wengine kusubiri kutokana na chaguo la kocha.

“Mimi niko tayari kushindana nao, sijawahi kucheza nao ila nina uhakika ni wachezaji wazuri wataongeza kitu kwenye timu,”amesema Phiri.

Simba ina washambuliaji wanne, Habib Kyombo, John Bocco, Jean Baleke, na Moses Phiri.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x