Phiri yupo sana Simba – Ahmed

MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amezima tetesi za mshambuliaji Moses Phiri kutaka kujiunga na Yanga SC.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo wa Jumapili dhidi ya Yanga, Ahmed amesema nyota huyo ataondoka klabuni hapo endapo klabu yake itaamua kufanya hivyo.

“Moses (Phiri) ataondoka Simba siku tukiamua kuachana naye na siku hiyo siioni, hawatampata ‘General’ hata siku moja,”

“Kwanza Moses Phiri anaondokaje Simba. Simba ni sehemu ya wachezaji kutimiza malengo yao, wachezaji wetu ni matajiri, wanaishi maisha ya kifalme.”amesema Ahmed.

Habari Zifananazo

Back to top button