Picha za Ronaldo zaondolewa Trafford

Mshambuliaji wa Manchester United amezidi kuingia kwenye vichwa vya habari, baada ya leo picha zake kung’olewa kwenye kuta za Uwanja wa Old Trafford wa timu hiyo uliyopo jiji la Manchester.

Katika baadhi ya picha na video, zimeonekana baadhi ya wataalamu wakiwa juu ya uwanja huo wakichana na kung’oa bango kubwa lililokuwa na picha ya mchezaji huyo.

Hatua hiyo inakuja zikiwa zimepita siku tatu tu tangu Ronaldo alipochafua hali ya hewa kwa madai ya kuwa timu hiyo imekosa mwelekeo tangu alipoondoka kocha Alex Ferguson mwaka 2013.

Katika mahojiano ambayo Morgan ameyaweka hadharani amesikika Ronaldo akiwaongela vibaya baadhi ya viongozi wa United, akiwemo kocha Eric Ten Hag ambaye alisema hawezi kumheshimu kwa kuwa yeye hamheshimu.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x