‘Pikipiki zitumike kwa shughuli za kilimo’

SERIKALI mkoani Tanga, imepiga marufuku pikipiki zilizotolewa na Wizara ya Kilimo kwa ajili ya kusimama shughuli za kilimo kutumika kama bodaboda, badala ya kwenda kuhamasisha kilimo biashara kwa wakulima.

Hayo yamesemwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashim Mgandilwa wakati wa ugawaji wa pikipiki 198 kwa ajili ya maofisa ugani wa wilaya tatu zilizopo mkoani humo.

Amesema lengo la vitendea kazi hivyo ni kuimarisha kilimo biashara, kiweze kuleta tija kwa wakulima sambamba na kuimarisha uchumi wa nchi na sio kutumika kwa matumizi mengine.

“Niwaagize Wakurungezi mkasimamie pikipiki hizo ziweze kuleta matokeo chanya kwa wakulima kama ambavyo lengo la serikali la kuleta Mapinduzi ya kilimo liweze kufikiwa na sio kutumika kwa shughuli za bodaboda,” amesema DC Mgandilwa

Nae Kaimu Katibu Tawala sehemu ya uchumi na uzalishaji mkoani hapa, George Mmbaga amesema kuwa mkoa huo ulikuwa upokee jumla ya pikipiki 377, lakini awamu ya kwanza zimekuja hizo 198

Ofisa ugani wa wilaya ya Handeni Chiza Kamele, amesema kuwa pikipiki hizo zinakwenda kumaliza changamoto ya uhaba wa vitendea kazi kwa maofisa ugani ngazi za kata hadi vijiji.

“Kwa vitendea kazi hivi sasa tunakwenda kuleta mapinduzi ya kilimo kwa wananchi, kwani tutaweza kuwafikia kwa wakati na kutoa elimu ya kilimo, ili waweze kupata mazao yenye ubora, “amesema Kamele.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x