Pilato wa Simba dhidi ya Al-Ahly huyu hapa

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limemtangaza Abongile Tom kuwa mwamuzi wa mchezo wa Simba dhidi ya Al-Ahly Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mwamuzi huyo raia wa Afrika Kusini kuwa ndiye atakayechezesha mchezo huo Ijumaa ya Machi 29.
.
Hii itakuwa mara ya tatu mchezo wa Simba kuchezeshwa na mwamuzi huyo, mara ya kwanza ilikuwa Desemba 2023 Mnyama akiwa ugenini (Morocco) alipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Wydad Casablanca.

Mechi nyingine ilikuwa Oktoba 16, 2022 Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 uwanja wa Mkapa.

Abongile aliwahi kuchezesha mchezo wa Yanga ambao waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Rivers United ya Nigeria.

Habari Zifananazo

Back to top button