Pinda aipa darasa Costech

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, ameishauri Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), iangalie namna ya kufadhili tafiti zenye kupeleka teknolojia kwa wakulima ambao bado wanahangaika jinsi ya kuongeza thamani ikiwemo kupata soko sahihi.

Pinda amesema alipotembea banda la tume hiyo katika Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale vilivyopo jijini Mbeya.

Pia Pinda ameishauri tume hiyo kufikiria kuanzisha wiki ya matokeo ya tafiti zenye tija kwenye jamii kwa kushirikiana na Taasisi za Utafiti na Vyuo Vikuu, huku akiipongeza serikali kupitia costech kwa kuendelea kufadhili Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Kituo cha Tengeru kutokana na mradi wa uzalishaji wa migomba maabara kwa njia ya chupa.

Kuhusu uzalishaji huo kwa njia ya chupa, Mtafiti kutoka TARI Tengeru, Benjamin Bitalibube amesema mpaka sasa imeshapeleka Miche ya migomba zaidi ya elfu 30 kwa wananchi wa mikoa mitano ya Mbeya, Arusha, Morogoro, Kilimanjaro na Kagera, huku wananchi wakipata elimu juu ya Kilimo cha migomba.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button