‘Pitieni banda la PURA mjifunze mengi’

MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), imesema itatumia Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kuelezea wananchi miradi wanayosimamia na tafiti walizofanya kwenye mafuta na gesi asilia.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa PURA Mhandisi Charles Sangweni alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la PURA lililopo katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam na kuwaomba wananchi wapitie kwenye banda lao kupata taarifa mbalimbali.

Ametaja miongoni mwa miradi hiyo kuwa na ule wa kubadili gesi waliyogundua katika Bahari kuu na kuweka kwenye hali ya kimiminika.

Amesema gesi iliyopo nchini inazalishwa kutoka Songosongo, Mnazi Bay na Kwara na imekuwa ikitumika katika kuzalisha umeme wa viwandani, majumbani na kadhalika.

PURA inafanya kazi ya kuishauri serikali juu ya masuala mbalimbali yanayohusu mkondo wa juu wa petroli pamoja na kusimamia shughuli zote za kusindika gesi asilia kuwa kimiminika.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button