IMERIPOTIWA kocha mpya wa Chelsea, Mauricio Pochettino amethibitisha nyota Joao Felix hayupo kwenye mipango yake.
Taarifa kutoka vyombo mbalimbali vya habari Ulaya Vimemnukuu Rais wa Atletico Madrid, Enrique Cerezo akisema kuwa nyota huyo mreno atarejea kikosini hapo baada ya mkataba wake wa mkopo kumalizika huko Chelsea.
Felix alijiunga na Chelsea kwa mkopo wa miezi sita mwezi January mwaka huu na alitarajiwa labda angeongezewa kandarasi ya kukipiga kwa matajiri hao wa London lakini ujio wa kocha Pochettino umetibua mipango hiyo.
Tangu amejiunga na Chelsea Jao Felix amefunga mabao manne kwenye timu hiyo.
Comments are closed.