Pogba ahismamishwa Juventus
#ITALIA: Kiungo wa Juventus, Paul Pogba amesimamishwa kwa muda kwa kosa la kuhusishwa na matumizi ya dawa za kusisimua misuli.
–
Uamuzi huo umethibitishwa rasmi na taarifa ya mahakama ya Kitaifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya nchini Italia.
–
Juventus imethibitisha kupokea taarifa rasmi kutoka kwa Mahakama ya Kitaifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya kuhusu hali ya Pogba.
–
“Pogba amesimamishwa kwa kosa la kupinga matumizi ya dawa za kusisimua misuli, klabu itazingatia jinsi ya kuchukua hatua katika mchakato huo”, taarifa imeeleza.
–
Wakala wa mchezaji huyo, Rafaela Pimenta amesema: “Tunasubiri taarifa za kukanusha na hatuwezi kusema chochote sasa”
“Kwa hakika, Pogba hakuwahi kutaka kupindisha sheria naweza kuhakikisha hilo”, aliiambia Tuttosport.
–
Imeandaliwa na Mwandishi Wetu
–
Tembelea// epaper.tsn.go.tz kusoma zaidi.
–
Una maoni usisite kutuandikia.