POLAND imeahidi kutuma ndege zake nne za kivita za MiG-29 Ukraine, ikiwa ni nchi ya kwanza ya NATO kufanya hivyo, katika hatua inayotajwa na Kyiv kuwa muhimu katika vita dhidi ya uvamizi wa Urusi.
Rais Andrzej Duda alisema ndege hizo kutoka kati ya zile (Polandi ilirithi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ujerumani ya zamani – zitatolewa katika siku zijazo.
“Linapokuja suala la ndege za MiG-29, ambazo bado zinafanya kazi katika ulinzi wa anga la Poland, uamuzi umefanywa kwa kiwango cha juu, tunaweza kusema kwa ujasiri kwamba tunatuma MiGs Ukraine,” Duda alisema.