JESHI la Polisi nchini limesema video fupi inayoonekana ikisambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonesha askari polisi akichukua fedha kwa raia wa kigeni, tayari ilishughulikiwa na askari huyo amefukuzwa kazi.
Akitoa ufafanuzi huo leo Septemba 14, 2022, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), David Misime amesema inawezekana wanaoisambaza video hiyo hawakupata mrejesho
Akitoa ufafanuzi huo leo September 14 msemaji wa Jeshi la Polisi nchini kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP), David Misime, amesema inawezekana wanaosambaza video hiyo hawakupata mrejesho wa hatua zilizochukuliwa dhidi ya askari huyo, aliyeendekeza tamaa.
Amesema ni kweli tukio hilo lilitokea Mkoa wa Kaskazini Unguja miaka mitano iliyopita, ambapo askari huyo alishtakiwa na ndani ya siku tatu alipatikana na hatia na alifukuzwa kazi, ili iwe fundisho kwa askari wengine wenye tabia kama hiyo.