Polisi Dar wakamata bunduki, bastola

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limekamata silaha mbili aina ya Shotgun Pump Action yenye namba MV 59787P iliyokatwa kitako na bastola aina ya Makarov yenye namba B.4135-1979 ikiwa na risasi tisa.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro kwa vyombo vya habari jana, ilisema jeshi hilo limefanikiwa kukamata silaha hizo kwa kushirikiana na raia wema.

“Silaha hizo zilisalimishwa eneo la Chamazi Vigoa na mtu mmoja ambaye amedai kuacha uhalifu akidai haulipi,” alisema.

Aidha, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limekamata watuhumiwa wanaojihusisha na matukio ya unyang’anyi na uvunjaji nyumba usiku na kuiba akiwemo Juma Hassan (23) mkazi wa Mji Mwema na wenzake 12.

Watuhumiwa hao walikamatwa katika msako wa Juni 12 hadi Julai 11, mwaka huu wakiwa na vitu mbalimbali vya kielektroniki vya wizi ambavyo ni televisheni aina mbalimbali 13, redio mbili, kompyuta mpakato mbili na meza moja ya televisheni na baadhi ya watu walioibiwa wametambua mali zao.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x