JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewatunuku vyeti vya sifa na zawadi askari wake 78 waliofanya vizuri kwa mwaka 2022.
Askari hao wamekabidhiwa vyeti hivyo jana na kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Muliro Jumanne Muliro katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Mafisa wa Polisi jijini hapo.
Muliro alisema askari hao wamefanya kazi nzuri ya kuweka mkoa wa Dar es salaam katika hali shwari na pongezi hizo za kijeshi ni kuanzia kwa maofisa hadi askari wa chini.
Kamanda alisema askari wa jeshi la polisi walijitahidi kuhakikisha hali ya usalama kwa mkoa huu inazidi kuwa shwari kutokana na fikra ambazo zimejenga na baadhi ya watu kwamba dar es salaam lazima kuwe na uharifu hususani siku za sikukuu krismasi na mwaka mpya.
“Askari wote walisema haiwezekani na hata vilivyojitokeza vikundi vya uharifu Askari hawa walifanya kazi kubwa kwa kushirikiana na raia kudhibiti vitendo hivyo na kwa ujumla dar es salaam ikaendelea kuwa salama,” Alisema Muliro.
“Kutokana na hivyo tukasema tuwe na wawakilishi kila eneo ambalo kazi hizi zinafanyika na kwa Askari ambao wamefanya vizuri zaidi, askari wote wamefanya vizuri lakini waliofanya vizuri zaidi tuwatambue kijeshi na kuwakabidhi zawadi ambazo ni kumbukumbu kwa sisi tuliopo na wanaokuja kwamba hawa Askari ni miongoni mwa Askari waliolifanyia vizuri jeshi la polisi na wananchi kwa ujumla kwa mwaka 2022,” Alisema Muliro.
Aliongeza kuwa miongoni mwa vigezi vilivyotumika katika kuwapata Askari hawa ni nidhamu, uaminifu,uweredi,ujasiri,kujituma, kupenda kazi yao, kauli kwa wateja, na huduma nzuri kwa wateja.
Aidha alisema siku za nyuma jeshi la polisi lilikuwa likilalamikiwa kwamba kauli zao zipoje lakini hivi sasa kuna mabadiliko makubwa sana.
“Dhahiri tunaona malakamiko dhidi ya Askari wa kanda maalum ya Dar es Salaam yamepungua kwa kiwango kikubwa sana vigezo hivyo vinaonekana vinazingatiwa ndio maana tunawatia motisha Askari ili watende kama hawa tuliowapatia zawadi hizi,”Alisema Muliro.
Muliro aliwataka Askari wa jeshi hilo kuendelea kufanya kazi zao kwa uharifu wakati wanapotimiza majukumu yao ya kazi.
Ugawaji wa vyeti hivyo ulienda sambamba na gwalide maalum la kutunuku sifa na zawadi lililokaguliwa na Kamanda wa jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Muliro Jumanne Muliro.