Polisi Dodoma wajivunia oparesheni zao
DODOMA;Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya kudhibiti Dawa za kulevya Kanda ya Kati Mzee Kasuwi leo Mei 03, 2024 amekabidhi silaha mbili 2 aina ya Gobole kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
Silaha hizo zimekamatwa katika oparesheni iliyofanyika Aprili 24 hadi 28 katika Wilaya ya Chamwino na Dodoma mjini ambapo zilikuwa zinamilikiwa kinyume cha sheria na zilikuwa zinatumiwa na baadhi ya watuhumiwa kulinda mashamba ya bangi.
Aidha, kupitia operesheni hiyo imefanikiwa kuteketeza ekari 9.5 za mashamba ya bangi, kilogramu 156 za bangi na misokoto 127 ya bangi.
Pia, watu 16 wanashikiliwa kuhusika na dawa hizo za kulevya na watafikishwa mahakamani baada ya taratibu za kisheria kukamilika