JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema linachunguza tukio la kifo cha Mtu aitwae Joel Misesemo Chizi anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 35 hadi 40.
Joel, Mkazi wa Mwananyamala akijihusisha na shughuli za ushereheshaji ‘MC’ na unasihi ‘concelor’ alijirusha kutoka ghorofa ya saba kwenye jengo la Derm Plaza lililopo Makumbusho Kijitonyama na kufariki.
Taarifa ya Jeshi la Polisi iliyotolewa leo Mei 23, 2023 inasema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa marehemu alionekana katika jengo hilo leo majira ya saa kumi na moja alifajiri na alimwambia Mlinzi wa zamu kuwa anaenda kufanya ibada kwenye Msikiti uliopo ghorofa ya 15 dani ya jengo hilo lakini muda mfupi baadaye alijirusha.
Taarifa ya Polisi imesema camera za jengo hilo zimemuonesha akijirusha kwa makusudi kutoka ghorofa ya saba kupitia dirishani na kufariki ambapo tayari mwili wake umepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi.
Jeshi la Polisi limepata gari la Marehemu aina ya Suzuki rangi ya silver lenye namba za usajili T142 DRM lililokuwa limeegeshwa kwenye maegesho ya magari katika eneo hilo na sasa limehifadhiwa Kituo cha Polisi