Polisi, TIA zashirikiana kuokoa mali za serikali
BAGAMOYO, Pwani: KATIKA kuokoa mali za serikali kwa kuokoa ajali za barabarani madereva wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wameanza kupewa mafunzo na Jeshi la Polisi.
Mafunzo hayo yanatokana na kuitikia agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alilolitoa Septemba 23, 2023 wakati akizungumza na madereva na kusisitiza ushirikiano kati ya madereva na waajiri.
Mafunzo hayo ya siku nne yamezinduliwa leo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani kwa ushirikiano kati ya TIA na Jeshi la Polisi Tanzania na kwa awamu ya kwanza itajumuisha madereva 18.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Ralph Meela amesema yanalenga madereva kufanya kazi vizuri kwa kuwa wamebaini madereva wengi hushindwa kuhudhuria mafunzo kwa kukosa muda.
Amesema Jeshi hilo liko tayari kutoa mafunzo kwa madereva palepale watakapokuwa wamekusanyika Kwa mfano viongozi wao wakiwa bungeni hivyo wao kutumia muda huo kupewa mafunzo.
Amezitaja mada watakazofundishwa kuwa ni pamoja na utambuzi wa kazi ya udereva,Mawasiliano na huduma Kwa mteja,kujitambua na maadili ya kazi,ulinzi na namna ya kujilinda pamoja na masula ya kijinsia.
Soma pia: https://habarileo.co.tz/polisi-iringa-wanolewa-udereva/
Kwa upande wake Mkuu wa TIA,Profesa William Palangyo amesema wanafundisha kuhusu ustaarabu na weledi wa kazi yao. Mafunzo hayo yanawakumbusha madereva kuokoa mali za serikali kwa kuokoa ajali.
Dereva anayepewa mafunzo hayo,Silvanus Nchimbi kutoka Taasisi ya TIA Mbeya amesema ni mafunzonyatakayowasaidia kufanya kazi kwa weledi na kutunza vyombo vya taasisi.