KAMANDA wa Kamanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Muliro Jumanne amesema alikuwa akiwahimiza vijana wa jeshi la polisi kufanya mazoezi ili kutunza afya zao akiwatolea mfano Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi ambaye licha ya umri wake ila alifanya mazoezi.
“Kama mzee yule mwenye miaka ile alikuwa akiweza kutembea, kukimbia kwahiyo tulikuwa tunawapa changamoto askari kijana wa miaka 23 miaka 30, miaka 45 kwamba lazima uwe na afya njema ili uweze kutekeleza majukumu yako”.amesema ACP Muliro.
Akizungumzia mafundisho aliyopata kwa kiongozi huyo, ACP Muliro amesema alijifunza pia uwajibikaji kwamba usipowajibika utawajibishwa.
–
“Kwahiyo hiyo ilikuwa ‘case study’ kwenye masomo mbalimbali ya kiuongozi, ambayo inatumiwa kesi ya Mwinyi kwamba ukipewa jukumu la kufanya kazi au kusimamia eneo fulani lazima utekeleze vizuri kwa kiwango cha juu, uzizingatie sheria, mifumo ya kiutendaji kinyume cha hapo unaweza ukawajibika au kuwajibishwa”. Amesema Muliro.