Polisi wakamata simu 61 za wizi, pikipiki, pombe haramu

SHINYANGA: JESHI la polisi mkoani Shinyanga limekamata simu 61 zilizokuwa zikimilikiwa na wanawake ambao wanajihusisha na wizi maeneo tofauti ya kwenye minada ya Kahama na Mwanza kwa kipindi cha wiki tatu kuanzia Novemba hadi Desemba mwaka huu.
Kamanda wa polisi mkoani hapa, Janeth Magomi amesema hayo leo alipozungumza na waandishi wa habari ambapo alisema doria ilianza kwa kuelekea Krismasi.
Kamanda Magomi amesema wamefanikiwa kukamata lita 173 za pombe haramu, mafuta ya dizeli lita 260 na pikipiki saba ikiwemo na vyuma tisa vya kuchimbia visima.
 
“Tumekata vifaa mbalimbali vya kupiga ramli chonganishi ikiwemo mkia udhaniwao wa mnyama Nyumbu ,kipande kimoja Cha ngozi ya mnyama adhaniwao ni simba.”amesema Magomi.
Katika kipindi hicho pia kamanda Magomi amesema walikamata makosa 2806 yaliyotokana usalama barabarani na kati ya hayo makosa matano yalikamatwa kwa kusababisha ajali.
 
“Kikosi cha usalama barabarani kinaendelea kutoa elimu kwa makundi yote na kusisitiza madereva kufuata sheria.”amesema Magomi.
Kamanda Magomi amesema wamefanikiwa kufikisha kesi nane mahakamani ambapo kesi moja ilikuwa ya ubakaji na mtuhumiwa amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.
1 comments

Comments are closed.