Polisi, wanahabari mambo safi

DAR ES SALAAM: kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu 2024 pamoja na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC), wamefungua ukurasa mpya wa ushirikiano katika kazi.

Pia, pande hizo zimekubaliana kushirikiana katika kutoa elimu ya namna ya kujilinda hasa kwenye oparesheni maalumu. Ikiwemo kila pande kuheshimu misingi, maadili ya kazi za kila mmoja.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika mjadala kuhusu usalama wa waandishi wa habari uliyoratibiwa na Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, , Mtatiro Kitinkwi amesema jeshi hilo linathamini kazi kubwa inayofanywa na wanahabari katika kuibua taarifa mbalimbali kwa

“Jambo moja ni lazima kila pande itambue kwamba kwa sasa Jeshi la Polisi kupitia Mkuu wa Jeshi IGP Camilius Wambura, limekuwa likifanya maboresho makubwa na hata leo kuwepo kwa mjadaa huo ni sehemu ya maboresho.

“Yapo ambayo sisi kama Jeshi tunaongozwa na sheria za Jeshi la Polisi ikiwamo na maagizo ambapo ni sehemu ya utaratibu wa kawaida kabisa kwetu. Lakini kwa maana ya sasa tutaendelea kushirikiana nanyi kama wanahabari mna wajibu wa kuyasemea yale mazuri ya Jeshi lenu (Polisi) badala ya kuangalia mabaya tu.

“Sisi tupo tayari kushirikiana na hata tunapokuwa kwenye matukio maalumu tungependa kuwepo na utambulisho maalumu ili tuweze kuwatambua wanahabari kama njia ya kuwalinda ili waweze kutimiza majukumu yao kwa utulivu hasa tuwapo kwenye oparesheni maalumu,” amesema Kitwinku

Kwa upande wake Mwenyekiti wa DCPC, Samson Kamalamo, amesema kuwa suala la ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na waandishi wa habari ni muhimu na kupitia DCPC itaendelea kuratibu hilo kama njia ya kumlinda mwandishi wa habari.

“Jeshi la Polisi linapaswa kumuona mwandishi wa habari kuwa si adui na nyakati zote hasa anapokuwa anatimiza majukumu yake, Polisi ana wajibu wa kumlinda ili aweze kutimiza majukumu yake,” amesema Kamalamo.

Nae, Mkuu wa Kituo cha Polisi Goba, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Maadili ya Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Pwani, Athuman Mtashi amesema kunapotokea operesheni maalum ni vyema polisi na wanahabari wakawasiliana na kuwa timu moja.

“Waandishi ni vema kuwe na mawasiliano ni upande upi ni salama wakae sio kuvizia tu Polisi na kuchukua matukio mabaya, ukikaa upande ambao si salama ni rahisi kudhurika,”amesema.

Makubaliano ya Polisi na Waandishi wa Habari yamekuja baada ya ripotiya Baraza la Habari Tanzania (MCT) iliyotoka mwaka jana kuonyesha kuwa katika kipindi cha miaka 10 toka 2013 hadi 2022, vyombo vya habari 94 vilikumbwa na madhila ikiwemo matamshi au vitendo 19 vilielekezwa kwa waandishi na vyombo vya Habari kwa ujumla.

Ripoti hiyo ilionyesha waandishi wanahabari 272, kati yake wanaume 219 na wanawake 53 walikumbwa na madhila mbali mbali katika kipindi cha miaka 10.

Kanzidata hiyo ya MCT inaonyesha kuwa taasisi iliyoongoza kwa matukio mengi dhidi ya uhuru wa habari ilikuwa ni polisi ambayo ilikuwa na matukio 51.

Habari Zifananazo

Back to top button