Polisi yadaka bodaboda wasumbufu 127
POLISI Mkoa wa Arusha imeendesha operesheni maaalum, ambapo waendesha pikipiki 127 pamoja na pikipiki 125 zilikamatwa kwa makosa mbalimbali, ikiwemo taa ambazo zimepigwa marufuku, namba bandia, pamoja na pikipiki ambazo zimefutwa namba.
Akitoa taarifa hiyo hii leo Desemba 14, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishina Msadizi wa Polisi, ACP Justine Masejo, amesema pikipiki hizo zimekuwa kero kwa wananchi, husasani wenye magonjwa mbalimbali na kwamba watuhumiwa watafikishwa mahakamani.