Polisi yadaka ‘Wafu 11′ Katavi

Kamanda Polisi Mkoa wa Katavi, Ali Makame

JESHI la Polisi mkoa wa Katavi linawashikilia watu 11 wanaodaiwa kujihusha na uhalifu wanaojitambulisha kwa majina ya Damu Chafu, Mazombi, Manyigu, Kaburi Moja na Wafu.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kuendesha vitendo mbalimbali vya kihalifu, ikiwemo uporaji wa simu, fedha kwa kutumia silaha za jadi.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Ali Makame, amesema makundi ya vijana hao hufanya uhalifu huo katika kumbi za starehe, misibani na barabarani pale wanapokutana na watu hasa nyakati za usiku.

Advertisement

Amesema vijana hao hutumia silaha za jadi kama vile visu,nyembe, panga, bisibisi na mawe.

Kamanda Makame amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Frank Martin (21), Mathias Edwin (18), Michael Richard (15), Moses Jairo (22), Jastin Patrick (27), Cosmas Titus (17), Salvatory Zakaria (22), Abel Patrick (32) John Benito (32), Joseph Seleman (21) na Raymond Godfrey (14).

Amesema vijana hao ni wakazi mtaa wa Nsemulwa, Kazima na Majengo, huku akisemaupelelezi bado unaendelea, ili kubaini mtandao mzima wa makundi hayo na mara, baada ya kukamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.